WOSIA MZITO WA GOMES KWA MKUDE

“Mkude namuamini na naamini katika uwezo wake na kipaji, lakini ili uweze kufikia malengo unatakiwa kutumia muda mwingi kufanya mazoezi utafika mbali zaidi ya hapa ulipo sasa, kama amenielewa na kukubaliana na kauli yangu nina imani atakuwa bora na ataisaidia Simba,” anasema Gomes na kuongeza;
“Suala la kucheza kwenye kikosi cha Simba bado lipo kwenye mikono yake yeye mwenyewe Mkude.Lwanga (Tadeo), Sadio (Kanoute), Mzamiru (Yassin) na Erasto (Nyoni) wote ni wazuri kwenye kiungo lakini kila moja ana staili yake ya kucheza.”
“Kila mchezaji nimewahi kumpa nafasi ya kucheza hii inaonyesha nilikuwa naelewa umuhimu wao kikosini, shida ni kwa Mkude ambaye sijamtumia mara nyingi hivi karibuni kwasababu hajafanya mazoezi na timu muda mrefu,” anasema na kuongeza:
“Hakuna mchezaji ambaye hakuwa
na namba kwenye kikosi changu, ukiona mchezaji sijamtumia basi kashindwa
kunishawishi mazoezini na amekosa programu zangu kuelekea mchezo husika."

Post a Comment