BIASHARA UNITED WAMTUMIA SALAMU ALLY HAPI KIAINA

 Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 

UONGOZI wa Biashara United umeweka wazi kuwa kwa sasa vichwa vinawauma kuhusu suala la usafiri wa wachezaji wao kuelekea nchini Libya kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Tripoli.

 

Biashara United inatoa kilio hicho ikiwa kama ni salamu kiaina kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi ambaye aliwazawadia shilingi milioni kumi baada ya timu hiyo kuivimbia Simba na kutoka nayo sare katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Mchezo wa kwanza wa kusaka ushindi katika Kombe la Shirikisho raundi ya kwanza dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya utachezwa Oktoba 15, Uwanja wa Mkapa.

 

Seleman Mataso, Mwenyekiti wa Biashara United amesema kuwa kuhusu mchezo wao wa nyumbani hawana tatizo ila kinachowaumiza ni ule wa marudio nchini Libya hali ni mbaya.

Mataso alibainisha kuwa wanahitaji kufanya vizuri kimataifa ila hali ni tete kwenye upande wa mkwanja.

“Hali ni mbaya sana kwa ajili ya mchezo wetu wa marudio ugenini, kwa muda huu gharama za matumizi ya safari mambo hayajakaa sawa na hata tiketi pia bado hatujapata hivyo wadau watupe sapoti katika hili,” .

Biashara United inayonolewa na Kocha Mkuu Patrick Odhhiambo iliweza kufika katika hatua hiyo baada ya ushindi mbele ya Dikhil.Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Oktoba 23 nchini Libya.

 

No comments