BENARD MORISSON AWAKA KUTOITWA GHANA



  

 

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Ghana na Klabu ya Simba, Bernard Morrison amelalamikia kitendo cha Kutoitwa Kwenye Kikosi Cha timu ya Taifa ya Ghana 'Black Stars licha ya kucheza vizuri akiwa na kilabu yake ya Simba SC.

 

Mshambuliaji huyo amelalamikia kitendo cha kuitwa kwa nahodha wa Black Stars, Andre Ayew ambaye kwa sasa anacheza soka huko Qatar kwenye nchi ambayo inachukuliwa na wengi kama sehemu ambayo wanaenda kucheza wachezaji waliostaafu soka na huku yeye anayecheza soka la ushindani zaidi yake ameachwa.

 

Morrison amesema akiitwa kwenye kikosi cha Ghana anaweza kufanya vizuri zaidi kuliko wachezaji wanaocheza Qatar lakini wanaitwa Black Stars na huku ikijulikana kabisa mchezaji pekee wa Qatar katika Kikosi cha Black Stars ya sasa ni nahodha Andre Ayew,

"Ninaweza kufanya kazi nzuri kuliko wavulana wengi wanaocheza Qatar. Kama unaweza kuwaita wachezaji wanaocheza Ligi za Qatar, kwanini mimi nisiitwe ? ,Tunacheza mpira wa levo moja, inaonekana ni aibu kwetu kucheza Afrika "

"Ndio maana nazikubali nchi kama Zambia, Misri na Afrika Kusini kwa Sababu wanaita wachezaji wote wanaostahili sio kwa kuangalia tu wale wanaocheza nje ya Afrika, kwa Black Stars wanawaita wachezaji wanaocheza Ndani ya Afrika ambao ni Magolikipa tu "

"Makocha waliopita walikuwa wanawaita Wachezaji wanaocheza Ligi za Afrika na ndio maana waliweza kwenda mbali zaidi, Hatuwahitaji hawa Makocha wa kigeni (Nje ya Afrika) ambao macho yao huwa Ni kwa Wachezaji wanaocheza Ulaya tu "

" Ninaamini sisi (tunaocheza Ndani ya Afrika) huwa tuna ari ya kulipambania Taifa Kuliko wao. "

 

 

 

No comments