𝐓𝐔𝐙𝐎 𝐙𝐀 𝐓𝐅𝐅 2020/21 𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎

 Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na nje

Hafla ya utolewaji tuzo kwa waliofanya vizuri katika michuano ya TFF msimu wa 2020/21, itafanyika leo Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Simba mabingwa wa msimu huo wanatarajiwa kuzoa idadi kubwa ya tuzo kutokana na mafanikio makubwa waliyopata katika msimu huo.

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes yeye anapigiwa chapuo ya kushinda tuzo ya kocha bora baada ya kuisaidia Simba kutwaa ubingwa wa ligi kuu pamoja na kombe la FA.

Mlinda lango bora tuzo inatarajiwa kwenda kwa Aishi Manula wakati John Bocco yeye ni mfungaji bora huku akiwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi akishindania na Clatous Chama na Mukoko Tonombe.

Chama ambaye kwa sasa amesajiliwa na RS Berkane, anatarajiwa kushinda tuzo ya kiungo bora akishindanishwa na Feisal Salum na Mukoko Tonombe wa Yanga.

Beki bora wanashindana Shomari Kapombe na Mohammed Hussein pamoja na Dickson Job wa Yanga.

Mchezaji bora wa kombe la FA Luis Miquissone anachuana na John Bocco na Feisal Salum.

Pia kutakuwa na tuzo ya mhamasishaji bora, timu yenye nidhamu, mchezaji bora chipukizi pamoja na tuzo za Ligi ya Wanawake 'Serengeti Lite'

 

No comments