WAZIRI AWESU AWASILI BUKOBA, APOKEWA NA WAZIRI BASHUNGWA

 Waziri Bashungwa azindua redio akisisitiza Uhuru wa vyombo vya habari  kuendane na wajibu - Gazeti App

 

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewasili wilayani Bukoba mkoa wa Kagera tayari kwa kuiendeleza kazi, amepokelewa na mwenyeji wake Mhe. Innocent Bashungwa Mbunge Karagwe na Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Pamoja na ratiba maalum ya kuhudhuria fainali ya Bashungwa Cup leo jioni wilayani Karagwe pia atatembelea miradi mbalimbali ya maji ikiwa ni pamoja na chanzo cha mradi wa Maji Omururongo na ukaguzi wa mradi wa maji mjini Kayanga.

Aidha Kesho Wilayani Misenyi atafika kukagua na kujionea utekelezaji unaoendelea wa mradi mkubwa wa Maji Kyaka-Bunazi na mwisho mradi wa maji Kemondo.


 

No comments