WARAKA KWA WASOMAJI WA Ojuku1.blogspot.com



Mwandishi na mmiliki wa blog hii akiwa na Mwenyekiti wa zamani wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad katika ofisi yake Buguruni jijini Dar es Salaam miaka kadhaa iliyopita. Wakati huo, Maalium Seif ambaye sasa ni marehemu, alikuwa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. 

KUANZIA kesho Septemba 2, 2021, blog yako hii itakuwa ikikuletea makala za kijamii, michezo, siasa na mambo mengine yanayoizunguka jamii tunayoishi. Kama ilivyo ada, makala hizo, moja kila siku, zitalenga kufundisha, kuburudisha, kuonya na hata kutoa angalizo. Makala zitazingatia maadili yote ya uandishi wa habari, zikiongozwa na weledi wa hali ya juu. Mwandishi ni mbobezi katika eneo hilo.

Tunakaribisha maoni, ushauri na utaalamu zaidi wakati tukiendelea ku-test mitambo!

No comments