EWURA YASHUSHA BEI YA MAFUTA ILIYOPANDISHWA JANA
KAIMU Mkurugenzi wa EWURA, Godfrey Chibulunje leo, Septemba 1, 2021 ametangaza
kuwa bei ya mafuta iliyotolewa jana imebadilika na bei itakayotumika ni ileile
iliyokuwa ikitumika mpaka kufikia jana Agosti 31, 2021.
“Jana tulitangaza bei mpya ya mafuta ambayo ilitakiwa ianze
kutumika leo Septemba 1, lakini sasa bei hizo zimeoneka zikiendelea kupanda na
hata kwenye soko la dunia kwa sababu zingine ambazo zipo inaoneka bei
inaendelea kuwa kubwa.
“Kwa mantiki hiyo sasa tumepata maelekezo mahususi kutoka Serikalini
kwamba bei hizo zisitishwe na bei ziendelee kutumika zilezile zilizokuwa
zikitumia mpaka kufikia siku ya jana.
“Tume maalum imeundwa kuchunguza na kuangalia mwenendo mzima
wa upandaji wa bei,” Amesema Chibulunje.

Post a Comment