WAKIMBIZI KUTOKA AFGHANISTAN WAKATALIWA KWA MANDELA
HUKU hali ya usalama katika taifa
laoi ikiwa bado tete kutokana na kundi la wanamgambo wa Taliban kuchukua
madaraka, wakimbizi kutoka Afghanistan ambao wametapakaa dunia nzima,
wamekataliwa nchini Afrika Kusini.
Taifa hilo imara zaidi kiuchumi
barani Afrika, limesema haliwezi kuchukua jukumu hgilo kwa vile lina idadi
kubwa ya wakimbizi wengine wanaohitaji kuhudumiwa vyema.
Idara ya Uhusiano wa Kimataifa imesema wakimbizi wanaweza
kuhudumiwa vyema katika Nchi za kwanza walizowasili ambapo wengi wapo Pakistan.
Uganda na Rwanda ndizo nchi pekee za
Afrika zilizokubali kuwapokea wakimbizi toka taifa hilo ambalo limeishi kwa
vita kwa miaka mingi sasa.

Post a Comment