MAMA WA WAZIRI ALIYEFARIKI NAYE AFARIKI


Elias Kwandikwa,Waziri wa Ulinzi wa Tanzania afariki dunia - Pars Today

FLORA Andrea ambae ni Mama mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias Kwandikwa amefariki akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Kifo chake kimetokea mwezi mmoja tu tangu kufariki kwa Mtoto wake ambae alikua Waziri wa Ulinzi Tanzania Elias John Kwandikwa.

Mwanafamilia ambae pia alikua Katibu wa Kwandikwa Julias Lugobi amesema marehemu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la mapafu na alilazwa katika hospitali kwa muda wa wiki moja. 

 

No comments