VIFAHAMU VYAKULA AMBAVYO VIKICHANGANYWA VINAGEUKA KUWA SUMU

KILA binadamu ana
kile alichojaaliwa na Mungu. Siku zote anachoamua mmoja kula huenda kikawa sumu
kwa mwingine.
Chakula anachokula
mtu kinaenda sanjari na hali ya kiafya. Wengine huumwa hadi kusababisha
kupoteza uhai na hii ni baada tu ya kupendelea kuchanganya chakula.
Mtu mmoja anaweza
kula sawa na kwa urahisi, ila kwa mwingine kikageuka sumu.
Hali hii huchochewa
zaidi na matokeo ya baadae pale unaposhindwa kuweka mchanganyiko sahihi na
wenye afya zaidi .
Kila aina chakula
ina faida zake, ila kinapochanganywa kinaweza kusababisha shida kwa mtu.
Kwa watu ambao
wanataka kuchanganya lishe ili kupunguza unene na vichocheo vyake ni vyema
kushauriana na wataalamu jinsi ya kupanga lishe bora.
Mtaalam wa lishe wa
Nigeria Habiba Haruna ameiambia BBC kuhusu aina sita za chakula ambazo zinaweza
kuwa sumu kwa mtu yeyote.
Samaki na Maziwa
samaki

Samaki na Maziwa ni
vyakula vyenye virutubisho lukuki na kuvichanganya katika sehemu moja vinaweza
visiwe na uwezo wa kutengeneza virutubisho sahihi na hii inaweza kuleta shida
baadaye.
Mwili wa binadamu
hauhitaji vyakula vya aina tofauti vyenye kemikali za aina moja kuchanganywa.
Huweza kusababisha sumu itakayopelekea mtu kutapika na hata kuharisha.
Maji ya limao na
Maziwa
Maziwa na limao huwa haviwezi kukaa sehemu moja kwani vikichanganywa lazima maziwa yaweze kukatika.

Ikiwa mtu
atachanganya maziwa na maji ya limao anaweza kutengenezea sumu, vilevile
yanaweza kuleta shida katika moyo.
Karanga na Mafuta ya mzeituni

Karanga ina umuhimu
mkubwa sana katika mwili wa binadamu na hutumika katika sehemu nyingi sana.
Pia karanga ina
kiwango kikubwa sana cha protini na wanga, vilevile Karanga ni moja ya
virutubisho muhimu katika lishe, haswa kwa wale ambao wanataka kupunguza uzito.
Kwa mafuta ya
mzeituni yanamsaada mkubwa pia hasa katika masuala ya tiba kwa baadhi ya
magonjwa, lakini mchanganyiko wa mafuta hayo na karanga yanaleta shida ila
inashauriwa kutumika pale moja inapokosekana lakini sio kwa pamoja.
Dawa pamoja na
sharubati ya limao
limao
Kuchukua dawa na kuchanganya na kitu chenye gesi ina madhara makubwa, wataalamu wanasema kuwa kunywa dawa na soda kama fanta au Coca-Cola inaweza kukusababishia kifo kutokana tu ongezeko kubwa la gesi.

Ameongeza kwa
kusema kuwa limao au kinywanji chochote chenye gesi hakipaswi kuchanganywa na
dawa ni hatari.
Nyama na mayai
mabichi
mayai
Kuchanganya nyama
ambayo haijaungwa na mayai mabichi inaweza kusababishia matatizo katika mwili
wa binadamu.
Inaweza kuwa sumu kwa wengine, zingine zinaweza kusababisha kutapika na kuhara kwa sababu haifai kutumika hivyo.

Nyama mbichi inaweza kusababisha athari ikiwa usindikaji wake haufuatwi ili kupunguza kiwango cha virutubishi vilivyomo.
Mtaalamu anasema
kuwa mayai mabichi hayana virutubisho kwenye mwili wa binadamu, yakiwa bado
kwenye hali hiyo hayapaswi kuliwa mpaka pale yatakapochemshwa au kukaangwa ndio
hujenga mwili.
"Mayai mabichi
sio ya kuyaamini," Anasema Mtaalamu wa chakula kutoka Nigeria, Habiba
Haruna.
Wataalamu
wanashauri watu kula kile wanajua kitakuwa na faida na haitawasababishia
matatizo yoyote.
Kujaribu kitu kipya
kunaweza kuwa na faida kwa wengine lakini pia kunaweza kuwa na madhara.
Kuna aina nyingi
sana ya vyakula ambavyo vikichangwanywa vinaweza sababisha madhara.
Mtu anapaswa kuwa mwangalifu katika uchaguzi wa vyakula ni vyema aweke vyeme virutubisho na kuepuka kuvichanganya.

Post a Comment