VIONGOZI WA TAASISI MBALIMBALI NCHINI WATAKIWA KUHESHIMU MISINGI YA UTAWALA BORA
NA STEPHANO MANGO, SONGEA
VIONGOZI wa Taasisi mbalimbali wamekumbushwa kuheshimu misingi
ya utawala bora pindi wanapotoa huduma kwa waliowapa dhamana kwa kufuata
taratibu, kanuni na sheria za nchi ili waweze kuleta matokeo chanya kwa jamii
ambayo imekusudiwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji na Mshauri Mwelekezi Utawala
Bora Wakili Lawrence Chuma katika warsha ya Utawala Bora iliyofanyika katika
ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma hivi karibuni na
kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa utawala bora.
Wakili Chuma amesema viongozi wa taasisi mbalimbali wanatakiwa
kuzingatia sheria, kaninu na taratibu za utawala bora na uwajibikaji
katika kuwatumikia wananchi kwa lengo la kuwajengea misingi imara ya kuwabijika
na kushiriki kuijenga nchi yao katika nyanja mbalimbali.
“Viongozi mmepata dhamana ya kuongoza wananchi hivyo mnapaswa
kuzingatia misingi ya utawala bora kwa kutoa taarifa sahihi na kwa kutumia
lugha nyepesi ambayo itawezesha wananchi kuwa na uelewa wa kutosha”amesema
Wakili Chuma.
Wakili Chuma ameongeza kwa kusema utawala unaozingatia
demokrasia, uwajibikaji, ushirikishwaji, maridhiano, haki za binadamu na
utawala wa sheria unatoa fursa kwa wananchi kunufaika na rasilimali za nchi kwa
pamoja.
Kwa upande mwingine Wakili Chuma amewataka wananchi kuwajibika
kikamilifu katika suala zima la kulinda, kusimamia na kutunza rasilimali za
nchi ili ziweze kutoa huduma endelevu kwa vizazi vijayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali
la Millenium Art Group Mnung’a Shaibu Mnung’a ametoa wito kwa viongozi
kuwajibika kwa wananchi kwa kuwapa taarifa sahihi kwakuitisha mikutano ya
hadhara ambayo inatoa fursa kwa wananchi kujadiliana na kuamua kwa pamoja
katika kutekeleza mipango yao.
“Tunasisitiza sana viongozi kuitisha mikutano ambayo hailengi
tu kuwapa taarifa wananchi kuhuhsu michango na maelekezo mbalimbali “amesema
Mnung’a
Amesema wananchi wamekata tamaa ya kwenda kushiriki mikutano ya
hadhara kwa kujenga dhana ya kwamba kwenye mikutano hiyo agenda ni kupatiwa
taarifa za michango mbalimbali na maagizo ya jambo fulani.
Kufuatia hali hiyo Mnun’ga ametoa wito kwa viongozi wa taasisi
mbalimbali kuwajibika kutoa elimu kwa wanachi katika kuwashirikisha na kujadili
kwa pamoja mipango inayopangwa na serikali na utekelezaji wake ili wananchi nao
washiriki kikamilifu.
Millenium Art Group Shirika lisilokuwa la kiserikali
limeendesha mafunzo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Halmashauri ya
Wilaya ya Songea ambao nao wanatakiwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora.

Post a Comment