PATA KUMBUKUMBU JUU YA MJUSI WETU ANAYEINGIZA FEDHA UJERUMANI

MWAKA 1909 hadi 1913 watu 500 huko Tendaguru Lindi walihusika
kufukua mabaki ya mifupa ya kiumbe mkubwa sana. Mifupa hiyo ilikuwa na uzito wa
kilo 250,000 ilichukuliwa na kusafirishwa kwenda nchini Ujerumani ambapo iliunganishwa
na kupatikana kiumbe kamili ambacho kilikuwa na urefu wa kwenda juu mita 13
kiasi cha watu sita na urefu wa ardhini mita 22 (kiasi cha urefu wa watu kumi).
wajerumani wanaendelea kummiliki mjusi wetu na kupata pesa
nyingi kutoka kwa watalii.
Mifupa halisi imehifadhiwa Berlin Museum of Natural History
huko Ujerumani.
Pichani ni mfano wa mjusi mkubwa aitwae Dinasour akiwa
ametengenezwa kwa mabaki ya chuma Makumbusho Jijini Dar es Salaam na Mabaki ya
Dinasour wetu huko Ujerumani.
Chanzo JF.


Post a Comment