POLEPOLE, GWAJI BOY, SILAA KIKAANGONI DODOMA LEO

 Humphrey Polepole akiingia Bungeni | JamiiForums

HAMPREY Polepole, aliyekuwa mwiba kwa wana CCM enzi za Uenyekiti wa Dkt John Pombe Magufuli akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, leo ataonja joto ya jiwe kibao kitakapomgeukia na kujikuta akiwa kikaangoni akihojiwa na Kamati ya Maadili ya Wabunge wa CCM.

Wabunge wengine watakaohojiwa leo ni Askofu Josephat Gwajima (Kawe) na Jerry Silaa (Ukonga) ambao Bunge lilipitisha azimio la kuwasimamisha kwa mikutano miwili kutokana na tuhuma za kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Vilevile, Kamati imependekeza Askofu Gwajima kufikishwa mbele ya kamati ya chama chake CCM na kuhojiwa kuhusu mwenendo wake.

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilipendekeza Silaa asimamishwe mikutano miwili ya Bunge la Tanzania na avuliwe uwakilishi kwenye Bunge la Afrika (PAP) kwa madai kuwa anaweza kusema uongo akienda huko.

Kilichomponza Silaa ni kauli yake ya kutaka wabunge wakatwe kodi kwenye mapato yao, jambo lililoelezwa kuwa ni uongo, kwani wabunge wanalipa kodi.

Kwa upande wa Gwajima, atatakiwa kujieleza kuhusu kauli anazozitoa katika Kanisa lake la Ufufuo na Uzima kuanzia Julai 25 mpaka Agosti 15 kuhusu chanjo ya korona.


No comments