BARNABA AWAJIA JUU WANAOMTUKANA KWA KUVAA SKETI

 Inaweza kuwa picha ya Mtu 1, amesimama na ndani

MUZIKI ni biashara, lakini kuna watu hawajui. Mwimbaji mwenye sauti tamu masikioni, Barnaba, hivi majuzi aliachia picha akiwa amevaa nguo za kike, akidai ni biashara.

Lakini baadhi ya mashabiki, bila kujali kauli hiyo wamemvaa na kumpa maneno yasiyo na staha.

"Sijali watu wote wanaonitukana, kuna watu wenye heshima zao wamenipongeza kwa sababu wanajua ni biashara, na siyo kuvaa tu ili mradi," anasema msanii huyo ambaye pia anajulikana kama Mopao.

"Wanaokereka wataendelea kukereka maana Septemba hii nitavaa kila aina ya nguo za kike kama sketi, madera, vijora na nimeshatoa tenda kwa madesigners wangu Wolperstylish kunishonea nguo nyingi za kike," anasema Barnabaclassic.

 


No comments