NUGAZ: WAPE SALAAM, TUTAENDELEA KUWA PAMOJA

 BREAKING Afisa Mhamasishaji na Msemaji wa Yanga Antonio Nugaz, ametozwa  faini ya shilingi 500,000, kwa kosa la kufanya mahoji… – SPORTS NEWS

DAKIKA chache baada ya uongozi wa Klabu ya Yanga kutoa taarifa za kutoongeza mkataba na Ofisa wake wa Uhamasishaji, Antonio Nugaz, kijana huyo mwenye asili ya mkoa wa Tanga ameibuka na kusema hana kinyongo na ataendelea kuwa pamoja na timu yake.

Antonio Nugaz kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram amewashukuru viongozi na wanachama wa yanga kwa muda wote aliokuwa nao katika utumishi wake ndani ya klabu hiyo.

Uongozi wa Klabu ya Yanga, Leo Septemba 1, 2021 ulitoa shukrani kwa aliyekuwa mfanyakazi wake (Afisa Mhamasishaji) Juma Khatib Nugaz (Antonio Nugaz) kwa utumishi wake ndani ya klabu hiyo.

“Kwa udhati wa Moyo wangu naomba niwashukuru kuanzia uongozi wote wa Yanga chini ya mwenyekiti wetu Dk. Mshindo Mbette Msolla na Kaimu Katibu Mkuu Mpya Senzo Mbatha Mazingiza, wafanyakazi wenzangu wote kwa upendo wenu kwa kipindi chote cha miaka miwili niliyoitumikia 
@yangasc kwa moyo Mkunjufu na kujitoa kwangu, Mungu awabariki, awalinde na awape kila hitajio la nafsi zenu ili tuweze kuipeleka mbele Brand ya Yanga.

"Wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga ninyi mumekuwa na mimi kwa moyo mmoja Ahsanteni sana Nawapenda sana na niatendelea kuwa nanyi.

Tutaonana tena hivi Karibuni. Insha Allah.

No comments