MICHEZO YOTE MIWILI YA AWALI AZAM FC KUCHEZEA NYUMBANI

AZAM FC ambayo itashiriki
michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Msimu huu, itaanza hatua ya awali
kwa kucheza mechi zake zote mbili nyumbani.
Azam imethibitisha kuwa michezo
yote miwili ya hatua ya awali ya kombe la shirikisho Afrika (Caf Confederation
Cup preliminary Round ) dhidi ya Horseed FC ya Somalia itachezwa Tanzania.
Mchezo wa kwanza Azam FC
watakuwa nyumbani mchezo utachezwa Chamanzi kwenye uwanja wao wa Azam Complex na
mchezo wa marejeano timu ya Horseed FC itakuwa mwenyeji na mchezo wake utachezwa
katika uwanja wa Uhuru Stadium(zamani shamba la bibi)

Post a Comment