KUMBE KUSHUSHA TOZO NI ZUGA TU, KODI YA MITANDAONI YAJA

SIKU chache baada ya Waziri
wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba kushusha toizo za miamala ya simu na ada za
mitandao ya siku, kiongozi huyo amesema yeye na Timu yake ya Wataalamu
wanaendelea kujadiliana kuhusu namna ya kuweka Kodi kwenye Application za
Mitandao ya Kijamii.
Amesema Ofisi za Mitandao hiyo hazipo hapa nchini lakini zinapata Hela nyingi
sana kila unapoingia kwenye Mitandao hiyo wao wanapata Hela hivyo Serikali
inaangalia jinsi ya kuweka Tozo kwenye Mitandao hiyo ili ijikusanyie Hela za
kufanya Maendeleo.
Amesisitiza kuwa Serikali inaleta Maendeleo kwa kutegemea Kodi, usipolipa Kodi
Nchi haiwezi kuendelea unakuwa unakwamisha Maendeleo.

Post a Comment