MAREKANI YAIACHIA TALIBAN NGUVU ZA KIJESHI ZA ANGA KULIKO BAADHI YA NCHI ZA NATO

 A Taliban fighter poses in the cockpit of a C-130 Hercules transport plane that was left behind during the evacuation

MMOJA wa wapiganaji wa Taliban akifurahia akiwa ndani ya moja kati ya ndege za kijeshi walizozikuta baada ya Marekani kujiondoa nchini Afghanistan.

BAADA ya Jeshi la Marekani kujiondoa kutoka Afghanistan, miaka takriban 20 tangu ilipoenda huko, kikundi kinachochukua madaraka cha Taliban, kimeachiwa ndege za kijeshi nyingi na zenye uwezo kuliko baadhi ya nchi washirika za NATO.

Imeelezwa kuwa Taliban imerithi ndege za kivita 48, ikiwemo Black Hawks inayosifika kwa kasi na uwezo wake angani, pamoja na ndege rasmi ya mashambulizi aina ya A-29.

Kikundi hicho kilifanikiwa kuingia na kuteka ngome za kijeshi katika miji ya Herat, Khost, Kunduz and Mazar-i-Sharif, na Kabul.

An A-29 attack plane is surrounded by kit left behind by western forces as they retreated from Kabul airport

Ndege ya kushambulia aina ya A 29 ikiwa imetelekezwa pembeni ikiwa na mizigo ya askari wa nchi za magharibi


Baadhi ya wapiganaji wa kikundi hicho waliposti picha wakiwa wamepiga kwenye ndege hizo walizoteka. Hata hivyo, kazi kubwa kwa kundi hilo ni kuwatafuta wa kuendesha ndege hizo kwani wengi wameikimbia nchi hiyo.

Baadhi ya nchi za NATO ambazo zitazidiwa uwezo wa kijeshi angani ni pamoja na Albania, Bosnia, Estonia, Iceland, Latvia, Lithuania, Luxembourg, Montenegro, North Macedonia na Slovenia.

 

No comments