DC JOKATE AAMURU WAWEKWE CHINI YA ULINZI

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Jokate
Mwegelo ameagiza Polisi kuwaweka chini ya ulinzi kwa Viongozi wa
Chuo cha Lubando Training College kilichopo Mtaa wa Butiama, Kata ya Mtoni
Kijichi baada ya kubaini Chuo hicho kinaendeshwa kinyume cha Sheria.
DC Jokate ametoa agizo hilo wakati alipoungana na wataalamu
katika ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ambapo
aliambatana pia na Mkurugenzi-Uthibiti, Ufuatiliaji na Tathmini kutoka
NACTE Dkt. Joefrey Oleke.
Baada ya kufanya mahojiano na Mkuu wa Chuo hicho, DC Jokate
alibaini kuwa kwa muda sasa Chuo hicho kimekua kikitoa mafunzo bila kupata
usajili, pamoja na kutoa mafunzo kwenye mazingira yasiyo rasmi .
"Hamna kitu kibaya kama kufanya utapeli halafu ukadhani
hutagundulika, Serikali ina macho kila sehemu, NACTE kaeni hapa na Polisi,
lazima tupate 'information', Chuo hakijasajiliwa lakini hata mandhari yake
haistahili, kuna Watu wanatoa huduma ambazo kiuhalisia hawastahili kutoa,
tushirikiane katika ufuatiliaji, hawa wachukuliwe hatua kali huu ni
utapeli", alisema DC Jokate
Kwa upande wake Dkt. Jofrey Oleke amesitisha shughuli
zote zinazoendelea katika chuo hicho, huku akielekeza taratibu nyingine za
kisheria kufuatwa huku akisema kwa ukaguzi uliofanyika, chuo hicho
hakitambuliki NACTE wala VETA.

Post a Comment