LICHA YA JESHI KUONDOKA, MAREKANI ITAENDELEA KUHAMISHA RAIA WAKE

MAREKANI imesema itaendelea na zoezi la kuwahamisha Wamarekani
zaidi kutoka nchini Afghanistan licha ya Jeshi la Marekani kuondoka kabisa
nchini humo jana Jumatatu ambapo Mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani Jake
Sullivan kama aliyosema Rais Biden, amesema zoezi la uokoaji ndilo
lililobadilika kutoka oparasheni za moja kwa moja za kijeshi hadi oparasheni za
kidiplomasia.
Amesema Marekani ina makubaliano na Taliban juu ya kuwaruhusu
Wamarekani waliosalia Afghanistan kuondoka Nchini humo idadi ambayo ni chini ya
Watu 200 na kusisitiza kwamba Marekani itaendelea kutuma misaada ya chakula,
matibabu na aina nyengine ya misaada ya kibinadamu kwa Waafghani.
Hata hivyo amesema misaada mengine ikiwa ni pamoja ya
kiuchumi na maendeleo itategemea vitendo vya Taliban kama watatekeleza ahadi
walizozitoa kwa umma baada ya kuingia madarakani.

Post a Comment