HATIMAYE ALIYEKAA MOCHWARI MIEZI NANE AZIKWA RORYA
MZEE Wilison Ogeta aliyefariki na
kutokuzikwa kwa muda wa miezi nane kufuatia kuwepo kwa mgogoro wa ardhi baina
yake na tajiri mmoja aitwaye Thomas Lissa, hatimaye amezikwa leo katika eneo
lake kwenye tukio lililosimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka.
Baada ya kufariki kwa mzee huyo,
mwili wake umekaa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa muda wote huo.
Ilikuwa ni vilio na simanzi wakati mamiliya ikipokea Mwili wa
mzee Wilison Ogeta mkazi wa Kijiji cha Nyambogo kilichopo kata ya Kitembe
wilayani Rorya mkoani Mara.
Mkuu wa wilaya Rorya alilazimimika kuingilia kati ambapo
amehakikisha mwili huo unahifadhiwa kisha hatua zaidi zifuatwe kumaliza mgogoro
wa ardhi uliodumu kwa muda wa zaidi ya miaka sita.

Post a Comment