MVUTANO MKALI WA MAWAKILI KESI YA MBOWE

 Kiongozi wa chama cha CHADEMA Freeman Mbowe afikishwa mahakamani

MVUTANO mkali unaendelea katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumi Uchumi, jijini Dar es Salaam, baina ya mawakili wa upande wa Jamhuri na Utetezi katika kesi ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Kesi imesimama kwa dakika 30 kwa ajili ya mapumziko baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha hoja zao kuhusu mapingamizi matatu ya upande wa utetezi yaliyowekwa Septemba Mosi mwaka huu ambapo Mahakama hiyo itatoa uamuzi.

Mapingamizi hayo ni pamoja na hati ya mashitaka kukosa viashiria vya makosa, kushtaki watuhumiwa kwa kosa la kula njama na makosa mengine kinyume na utaratibu wa kuandaa hati ya mashitaka.

No comments