TSHABALALA AONGOZA KWA FOLLOWERS INSTA!

NAHODHA Msaidizi wa Simba,
Mohammed Hussein 'Zimbwe Junior' maarufu zaidi nchini kama Tshabalala, ndiye
mwanasoka mwenye wafuasi wengi zaidi katika mtandao wa Instagram kuliko wengine
wote.
Siri hiyo imefichuliwa na Kaimu Ofisa
Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, akisema wakati duniani yupo mshambuliaji
nyota Cristiano Ronaldo, hapa nchini tunaye Tshabalala.
"Kule Cristiano, huku
Tshabalala
Kwa taarifa tu; nahodha msaidizi
wa Simba SC Tanzania Mohamed Hussein "Zimbwe Jr" ndiye msakata ndinga
anayecheza Tanzania mwenye wafuasi wengi zaidi hapa Instagram. Sasa kafikisha
followers 893,000. Namba moja nchi nzima kwa wanasoka.
Ni matarajio yangu kampuni na
wadhamini wanaona takwimu kama hizi. Manchester leo wanaringa kumpata Cristiano
Ronaldo kwa sababu wafuasi wake Insta - nazungumzia watu milioni 333, sasa
wataanza kufuatilia habari za Man Utd.
Fursa ndiyo hii. Na kapteni
wangu huyu hana baya. Hana kashfa. Hana ukorofi. Mtu muungwana. Ni faida kwa
brand yoyote. Mtazameni kwa jicho la biashara!!!

Post a Comment