TOZO ZA MIAMALA ZASHUSHWA KWA ASILIMIA 30

Waziri wa Fedha na Mipango Dr.
Mwigulu Nchemba Leo August 31,2021 ametia saini marekebisho ya Kanuni za Tozo
za Miamala ya Kieletroniki za Kutuma na Kutoa Fedha za Mwaka 2021 na kupunguza
viwango vya tozo za miamala kwa 30% huu ukiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais
Samia ambaye alielekeza tozo zipitiwe upya baada ya kusikia kilio cha wananchi
kuhusu tozo hizo.
Serikali pia imefanya majadiliano na watoa huduma za simu
ambao na wameridhia kupunguza viwango vya tozo wanazotoza katika miamala ya
kutuma na kutoa fedha kati ya mtandao na mtandao mwingine kwa 10%.
Viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi kwa Tangazo la
Serikali kesho September 01,2021 ambapo Serikali imesema inaamini uamuzi huo
utatoa nafuu kwa wananchi na kuiwezesha Serikali kupata fedha za kutekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyokusudiwa wakati tozo hizo
ziliporidhiwa na kupitishwa na Bunge la Bajeti la Mwaka 2021/2022

Post a Comment