MBUNGE CCM AMCHARUKIA GWAJIMA

 UFAFANUZI: Kauli ya Mbunge Elibariki Kingu ”KUTEKWA NI JAMBO LA KAWAIDA”

KUFUATIA     mzozo kati ya Bunge na Mbunge wa Kawe kupitia CCM, Askofu Josephat Gwajima juu ya chanjo ya corona, mwakilishi wa wananchi kutoka Singida, Elibariki Kingu amekuja na maneno haya....

"Hichi anachokifanya Gwajima ni kiburi kilichojaa kuvimba na kulewa sifa za dunia na si sifa za kuwakilisha Mungu katika madhabahu.

"Askofu Gwajima ametoa tuhuma nzito kwa nchi, na mimi nimejiuliza maswali hivi ni kweli jeshi la polisi halioni "criminality" iliyopo katika kauli za Gwajima, hivi kweli jeshi la Polisi halioni hatari ya kauli za Gwajima kwamba zinaweza zikasababisha Serikali ikapinduliwa kwamba Rais ameamua kuuza watu wake.

"Adhabu zitakazotolewa kwa Askofu Gwajima kwa hili zisiishie hapo, hata huyu aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee hajawahi kutufanyia vitimbi vya namna hii, nshangaa sana kwanini Chama changu kimekaa kimya mpaka sasa.

"Rais Magufuli kama Mungu angekuwa amemtunza hai mpaka leo, Gwajima angeweza kufungua mdomo wake na kuleta hizi chokochoko, kama kuna mbunge anafikiri kwamba atatumia "forum" hii kwa sababu tu hakupendezwa na Rais Samia kuwa madarakani, Wallahi nakuambia tutadili nae,akitokea mmoja akataka kujenga umaarufu binafsi badala ya umaarufu wa taasisis na kulinda mifumo ya Taifa letu, kabla ya kuja kwako Spika, tutatwangana makonde huko."

 

No comments