SOMA HII UPATE KITU CHA KUMALIZIA WIKIENDI

Siku moja wakiwa wamekaa pamoja
mume pamoja na mke wake, mume akamwambia mke wake...
"Mke wangu nimewakumbuka
sana ndugu zangu (kaka zangu dada zangu na hata baba na mama) tujumuike pamoja
na kula pamoja
Kesho nitawaalika ili tujumuike
nao katika chakula cha mchana, itabidi uandae chakula kwa ajili yao."
Mke akasema kwa unyonge
"sawa mungu akipenda."
Asubuhi ya siku iliyofuata mume
akatoka kwenda katika mishughuliko yake lakini baada ya masaa kadhaa akarejea
nyumban na kumuuliza mke wake.
"Mke wangu umeandaa chakula
cha mchana kwa ajili ya wageni? maana baada ya lisaa limoja watakuwa
wameshafika."
Mke akajibu "hapana
sijapika kwani ndugu zako sio wageni hapa watakula chochote
watakachokikuta."
Mumewe akamwambia mungu
akusamehe mke wang kwa nini unayasema hayo ilihali tokea jana nilikuambia ya
kuwa wazazi wangu wanakuja
Na kwa nini hukunambia mapema
kuwa hutopika ilihali baada ya lisaa limoja wazazi wangu watakuwa hapa nini
unafanya mke wangu."
Mke akamjibu "waache waaje
nitawataka radhi, kwani wao si wageni hapa watakula chochote
watakachokikuta."
Basi mume ikambidi aondoke pale
nyumban kwa kukwepa fedheha.
Baada ya dakika kadhaa mlango
ukagongwa mke akaenda kuufungua...
Kwa mshangao mkubwa alipofungua
mlango akakuta wageni waliokuja hapo ni wazazi wake babaake, mamaake dada zake
pamoja na kaka zake
Akastuka kwa mshangao na
kuwakaribisha ndani,
Baba akamuuliza kuwa mume wake
yupo wapi?
Akajibu kuwa alikuwepo hapa
ametoka dakika chache kabla hamjafika.
Baba akamwambia "mumeo jana
alitupa taarifa kuwa leo anatuarika hapa tuje kula pamoja chakula cha mchana
sasa vipi yeye ametoka si busara."
Yule mwanamke akastuka kwa
taarifa hiyo na kuanza kujifikicha mikono yake huku akiipiga piga hali ya
kuchanganyikiwa."
Ikambidi aingie ndani na
kumpigia simu mume wake akamwambia "kwa nini hukuniambia kuwa wazazi wangu
ndio wanaokuja?"
Mumewe akamjibu "Wazazi
wangu na wazazi wako wote ni kitu kimoja/hawana tofauti."
Mke akamwambia "Lete chakula
huku chakula kilichokuwepo ni kichache haki tawatosheleza."
Mume akamjibu "Mimi nipo
mbali na hao si wageni watakula chochote kilichopo kama wewe ulivyokuwa ukitaka
kuwalisha wazazi wangu."

Post a Comment