RONALDO ASUBIRI KUREJEA MAN UNITED AKIWA KATIKA MJENGO WAKE WA BEI MBAYA JIJINI LISBON

WAKATI mashabiki wa
soka wakisubiri Cristiano Ronald kujiunga na Man United akitokea Turin kwa
Juventus, mkali huyo wa mabao amepumzika katika mjengo wake wa bei mbaya jijini
Lisbon.
Mjengo huo una
thamani ya pauni milioni sita, sawa na pesa ya madafu bilioni 18, ambao una kila
kitu ndani na kwa mujibu wa majirani, staa huyo hana mbwembwe na hawajawahi
kusikia watu wakila bata kwa pati kama mamilionea wengine wanavyofanya.

Post a Comment