POLISI WAZUIA KIKAO CHA KAMATI KUU NCCR MAGEUZI

TAARIFA ya Edward Simbeye ambae ni Mkuu wa Idara ya Uenezi wa chama hicho imesema polisi wamedai ni marufuku kwa vyama kufanya vikao vyovyote bila kibali maalum toka polisi.
" Polisi wenye silaha nzito na mabomu ya machozi, magari
matatu yamezingira ukumbi uliokuwa ufanyike kikao chetu cha Kamati kuu ya NCCR-MAGEUZI kwamba hakuna kikao chochote cha Siasa kinaruhusiwa
kufanyika bila kibali maalumu kutoka jeshi la Polisi.
Wamefunga geti la kuingia na kutokea eneo la Kikao hakuna mtu
kuingia ndani ya Kikao." Edward Simbeye

Post a Comment