JIFUNZE KITU KATIKA MAISHA YAKO

Kijana mmoja wa kiume alikuwa
akipita nyumba hadi nyumba akitafuta msaada wa chakuyla kutokana na njaa.
Alipitia nyumba nyingi, hatimaye akatokeza kwenye nyumba moja.
Alipobisha hodi, binti mzuri na
mrembo alifungua mlango, kijana badala ya kuomba chakula aliomba glasi ya maji.
Lakini binti yule akagundua kuwa mpiga hodi alikuwa ni mwenye
njaa, hivyo akampatia kikombe cha maziwa na viazi vitamu ambavyo kijana yule
alivifakamia kwa uchu.
Alipomaliza, akamuuliza mrembo
mbele yake "Unanidai kiasi gani kwa hichi ulichonipa?" binti alijibu
"Sikudai chochote kwani Mama alitufunza tusikubali malipo kwa Jambo la
fadhira" kijana alimshukuru sana kisha aliondoka.
Miaka Mingi ikapita yule binti sasa ni mwanamke, alipata
maradhi mabaya na madaktari wa sehemu ile walishindwa kumtibu na kushauri
apelekwe mjini kwa madaktari bingwa.
Alipofikishwa mjini katika ile
hospitali, akalazwa na taarifa za mgonbjwa yule zikamfikia daktari
aliyefahamika kwa jina la Rajab. Huyu alivutiwa na mgonjwa baada ya kutajiwa
anakotoka, kwani ni kwao pia yule daktari.
Alipokwenda na kumtazama,
akamkumbuka, lakini asimweleze chochote, akafanya kila alichoweza kuhakikisha
mgonjwa yule anapata nafuu. Jitihada kubwa ilifanyika na yule mwanamke alipona.
Dr. Rajab aliagiza ofisi impatie bill ya mwisho ya mgonjwa, aliitazama
na akaandika maneno machache kisha bili hiyo ikatumwa kwa mgonjwa.
Mgonjwa aliogopa kuisoma maana alijua anadaiwa pesa nyingi
sana na asingemudu kuzilipa zote. Kwa Kujing'ang'aniza sana alisoma, alikuta maneno
yameandikwa "billi yako imelipiwa kikamilifu na kikombe cha maziwa na viazi
vitamu".... Machozi yalimtiririka sana alipokumbuka tendo la fadhira
alilofanya siku za nyuma.
FUNZO
Ndugu Tendo lolote la fadhira unalolitenda halipotei,
hujirudia kwa namna tofauti hivyo tuweni watu wa kujitolea kwa ajiri ya wengine
, tuwe watenda mema, maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mwenyezi Mungu.

Post a Comment