PERFECT CHIKWENDE, MEDDIE KAGERE WATOLEWA KWA MKOPO

WACHEZAJI wawili wa kimataifa wa
klabu ya Simba, Perfect Chikwende na Meddie Kagere wametolewa kwa mkopo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
ndani ya Simba, wachezaji hao wametolewa baada ya kuafikiwa na kocha wao
Mfaransa, Didier Gomes da Rosa.
Kagere atarejea nyumbani kwao
Rwanda kujiunga na APR na Chikwende pia atarejea Zimbabwe kujiunga na klabu
yake ya zamani, FC Platinum.

Post a Comment