NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO KONDE, USHETU
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema Uchaguzi Mdogo katika Majimbo ya Konde (Mkoa wa Kaskazini Pemba) na Ushetu (Shinyanga) utafanyika Oktoba 09, 2021
Wagombea watachukua fomu kuanzia 13-19 Septemba, uteuzi
utafanyika Septemba 19 na Kampeni zitaanza 20 Septemba hadi 08 Oktoba.
Jimbo la Konde lipo wazi baada ya Mbunge Mteule kujiuzulu na
aliyekuwa Mbunge wa Ushetu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa , Elias
John Kwandikwa kufariki dunia Agosti 02 mwaka huu.

Post a Comment