MZEE ALIYEMBAKA HOUSEGIRL KORTINI JUMANNE 31 AGOSTI 2021

 Jinsi ya kuishi mahakamani kwa mhojiwa, mdai na ushahidi: maelekezo ya kina

MSHTAKIWA Sadalla Juma Sadalla mwenye umri wa miaka 74 mkazi wa Bububu, Unguja, atafikishwa mahakamani Vuga, Jumanne 31 Agosti 2021 kwa makosa ya kumbaka msichana wake wa kazi mwenye umri wa miaka 15 (jina limeifadhiwa).

Mshitakiwa Sadalla Juma Sadalla alifikishwa mahakamani mara ya kwanza Agosti 18, 2021 na kusomewa mashataka yake na kesi hiyo imepangiwa tena tarehe 31 Agosti 2021 katika mahakama ya Vuga mjini Unguja. Katika juhudi la kukomesha vitendo vya ubakaji na udhalalishaji visiwani Zanzibar, serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na vyombo vya ulinzi vinajitahidi kuwafikisha mbele ya sheria wale wote watakaotenda makosa hayo ya ubakaji na udhalalishaji.

Mshitakiwa Sadalla Juma Sadalla alilalamikiwa na wanaharakati visiwani Zanzibar kuwa ni mzoefu katika vitendo vya ubakaji pamoja na udhalalishaji na alipombaka msichana wake wa kazi mwenye umri wa miaka 15, alikuwa yupo huru na alipanga kuondoka unguja kukimbia kesi hiyo baadhi ya majirani zake walisika lakini vyombo vya usalama viliwahi kumshika na hatimaye kumpeleka mahakamani.Mshitakiwa Sadalla Juma Sadalla yupo mahabusu kwa kuwa shitaka la kubaka, udhalalishaji halina dhamana.


 

No comments