DENMARK KUFUNGA UBALOZI WAKE NCHINI

Waziri wa Mambo ya nje Jeppe Kofod alisema Upangaji huu upya
ni kusaidia juhudi za nchi hiyo inazofanya nyumbani na duniani ili kuleta
mabadiliko makubwa iwezekanavyo.
"Kipaumbele changu kama Waziri wa Mambo ya nje ni
kuhakikisha usalama wa watu wa Denmark katika ulimwengu ambao demokrasia, haki
za binadamu, na madili yetu vinakandamizwa."
Tanzania na Denmark zimekuwa na uhusiano mzuri katika miaka
iliyopita. Wanasiasa wengi, maafisa wa serikali, wanasayansi, wafanyabiashara,
viongozi wa dini na watendaji wa asasi za kiraia kutoka mataifa husika wameunda
uhusiano wa karibu na kushiriki mazungumzo yenye tija.
Tanzania ndiyo nchi ya kwanza ya Kiafrika ambayo Denmark
ilianzisha nayo ushirikiano wa kutoa misaada ya kimaendeleo mnamo 1963, muda
mfupi baada ya Tanzania (wakati huo Tanganyika) kupata uhuru.

Post a Comment