MCHUNGAJI, MKEWE WAFUNGWA MIEZI 18

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya
Bukoba imewahukumu Merchades Mugishagwe anayejiita Mtumishi wa Mungu kifungo
cha miezi 18 na faini ya shilingi million 3 na Mkewe Agripina Pius kutumia
kifungo cha nje kwa muda huo wa miezi 6 baada ya mahakama hiyo kuwatia hatiani
kwa kushindwa kutimiza majukumu yao kama wazazi.
Watu hao wawili walikuwa wanakabiliwa na mashitaka 8 yakiwemo
ya kushindwa kutimiza wajibu wao kama wazazi na kutowapeleka watoto wao watatu shule
waliokuwa wametimiza umri wa kwenda shule kwa madai ya kuwa Mungu wa Isaka na
Yakobo hatambui elimu ya dunia.

Post a Comment