ASKARI WALIOUAWA DAR WAAGWA

WAOMBOLEZAJI mbalimbali leo wameshiriki katika hafla ya
kuwaaga askari polisi wanne waliouawa kwa kupigwa risasi katika uwanja wa Kambi
ya Polisi, Kilwa Road ilipo Hospitali ya Polisi.
Askari hao waliuawa Agosti 25, 2021
katika majibizano ya risasi katika eneo la Oysterbay, Barabara ya Ali Hassan
Mwinyi, jijini Dar es Salaam.
Miili ya askari hao inaagwa leo Agosti 27, 2021 huku Mkuu wa
Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro akiongoza zoezi hilo.

Post a Comment