MBATIA ALISHUKIA JESHI LA POLISI

MUDA mchache baada ya
chama chake cha NCCR-Mageuzi kuzuiwa kufanya mkutano wake wa ndani na Jeshi la
Polisi, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, James Mbatia, amelishukia kwa
maneno makali jeshi hilo lililo chini ya IGP, Simon Sirro.
"Hata kama watatuua
sote hatuwezi kukubali serikali inavyondeshwa kibabe bila kufuata Katiba, kila
mtu kambale mamba masharubu tu hatuwezi kuendelea na mambo ya ajabu ajabu kama
haya, kwanini hata kauli ya Amir Jeshi Mkuu haiheshimiwi!?? Tanzania tunaenda
wapi??.
"Nasema kwa dhati kabisa kwamba hawa wanaozuia mikutano ya vyama vya
Upinzani wanachochea chuki na wanachochea hasira kwa Watanzania nyie ndio
Magaidi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania msiwasingizie wengine.
"Jeshi la Polisi mimi ni M/kiti wa Chama cha Siasa Tanzania nani asiyenijua
nawasiliana na IGP hajibu simu yangu, nawasiliana na RPC hawajibu simu zangu,
nyie ndio mnapandikiza chuki na mnaihujumu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Nchi imekuwa ya hovyo kabisa, Polisi mmeota masharubu mmeshindwa hata
kuheshimu kauli ya Rais kwamba vyama vinaruhusiwa kufanya mikutano ya ndani
sasa ni kauli ya nani itaheshimiwa katika nchi hii?? Sisi tuna hasira kweli
kweli Rais tunakuomba tuzungumze mdharau mwiba mguu huota Tende.
"Kama Jeshi la Polisi mmeamua kulianzisha sisi NCCR-Mageuzi tunaweza
kulimalizia, tumefanya siasa za kuunganisha nchi na kutafuta maridhiano kwa
muda mrefu ili kuisaidia nchi yetu ila mmeendelea kutuona wajinga mmekosa
uungwana mnataka kulivuruga Taifa hili, sisi tupo tayari kwa lolote kuanzia
sasa tumechoka kunyanyasika ndani ya Nchi yetu wenyewe.
"Nchi imejaa chuki, angalia mauaji aliyofanya Kijana Hamza watu
wanashangilia hii inaonesha dalili ya chuki kwa Taifa, tunatoa pole kwa Familia
za Marehemu wote ikiwapo Familia ya Hamza kwa kuwa na yeye ni binadamu na
tunawapa pole chama cha Mapinduzi kwa kuondokewa na kada wao Hamza ni kada wao
wasikatae sisi NCCR-Mageuzi tunawapa pole.

Post a Comment