MAPATO BANDARI TANZANIA YAONGEZEKA


 Dailynews


LICHA ya janga la ugonjwa wa Corona linaloisumbua dunia, bandari za Tanzania zimerekodi ongezeko la mapato kwa miezi sita  kutoka shilingi bilioni 525.4 hadi shilingi Bilioni 531.

Msemaji Mkuu wa serikali, Gerson Msingwa amesema, mapato haya si haba, kwenye kipindi cha Covid-19 zipo bandari nchi za wenzetu wamerekodi 0% ya mapato, Bandari zetu zimeendelea kufanya vizuri licha ya changamoto za Ugonjwa wa Uviko-19 Duniani”.

“Bandari yetu imeboreshwa kina kimechimbwa zaidi ili Meli kubwa zaidi ziweze kufika, kutokana na uwezekazaji huu Bandari yetu ya Dar es Salaam wiki tatu zilizopita imeandika rekodi kubwa kwa Bara la Afrika, ambapo kupitia gati maalumu ilifanikiwa kupokea magari 3743, na asilimia 65 ya magari hayo (magari 2945) yalikuwa yanapelekewa nje ya Nchi, mapato yameongezeka"——— 
@gersonmsigwa 

“Sasa nitakuwa nazungumza na Watanzania kila kiki Kwa taarifa fupifupi, teknolojia inaturuhusu sitowalazimisha waandishi kuja kwenye mkutano tutawaletea taarifa kwenye vyumba vyenu vya habari, itakuwa ni taarifa fupifupi na Watanzania watapata nafasi ya kuuliza maswali hata leo hapa baada ya maswali ya waandishi tutapokea maswali ya Wananchi Kwa njia ya simu”

 

No comments