MANARA SI MSEMAJI, ATAINGIA KWENYE KITENGO CHA UHAMASISHAJI- YANGA

UONGOZI wa Yanga umeweka bayana
majukumu ya Haji Manara aliyetambulishwa juzi akitokea klabu ya Simba
Kumekuwa na sintofahamu kuhusu
nafasi ya 'Bugatti' hasa ikizingatiwa Yanga inae Afisa wa Habari, Hassan
Bumbuli na Afsa wa Uhamasishaji Antonio Nugaz
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji
Mfikirwa amesema Manara ataingia kwenye Kitengo cha Uhamasishaji wakiamini
atasaidia kuimarisha kitengo hicho kuelekea Mabadiliko ya mfumo wa Uendeshaji
"Wakati tunamtangaza Manara
pale Serena Hotel hatukusema anakuja kufanya kazi gani hasa, lakini niseme
uongozi upo makini na haujakurupuka kumchukua Haji, kuna majukumu yapo na
ataenda kuyafanyia kazi hasa kutokana na mabadiliko ya klabu yanayofanywa sasa,
kutoka katika mfumo wa sasa na kwenda mfumo mpya na wa kisasa zaidi,
hatoingiliana na Nugaz na Bumbuli" alisema Mfikirwa
"Katika mabadiliko ambayo
tunayafanya kwa sasa kuna suala la ‘fan base', hapa tunahitaji mtu wa
kushawishi mashabiki waingie kwenye mfumo rasmi wa klabu baada ya kukamilika
taratibu zote, kuna mashabiki mikoa mbalimbali ambao klabu inawahitaji, lakini
lazima washawishike, hapa ndipo panapohitajika watu au mtu mwenye kujua
kushawishi, kuna nani zaidi ya Manara?, ili ni eneo ambalo tunaamini atafanya
kazi kubwa sana kwa manufaa ya klabu"
Mfikirwa alisisitiza kuwa kila
mmoja (Nugaz, Bumbuli na Manara), atafanya kazi yake kwa maendeleo ya klabu na
hakutakuwa na mwingiliano.
"Mashabiki wauamini uongozi
wao, sisi tupo pale (madarakani) kwa niaba yao, hivyo chochote tutakachokifanya
ni kwa faida ya timu hivyo hakuna haja ya kuwa na shaka na ujio wa Manara ndani
ya Yanga"

Post a Comment