KAULI YA SIRRO KWA WAZAZI WA HAMZA ZAKOSOLEWA

KAULI ya Inspekta
Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro juu ya kuwataka wazazi kutozaa watoto wa
hovyo kama walivyo wazazi wa Hamza Mohammed, kijana aliyewaua polisi wanne
kabla ya yeye kuuawa na polisi, imekosolewa na wadau mbalimbali nchini.
Hamza, kada wa CCM
na ambaye chanzo cha tukio lake bado hakijawekwa wazi na Polisi ambao bado wapo
katika uchunguzi, aliwaua polisi hao siku chache zilizopita, akipambana nao kwa
zaidi ya dakika 45.
Sirro, akizungumza
katika siku ya kuwaaga polisi waliouawa, alisema kijana Hamza ni matokeo ya
wazazi kuzaa watoto hovyo, hivyo akawataka wazazi wengine kutokuwa kama wa
Hamza.
Hata hivyo, makundi
ya wadau mbalimbali, wamemkosoa kiongozi huyo mkuu wa Jeshi la Polisi, wakidai
maneno yake hayakuwa sawa, kwani hakuna mzazi, akiwemo yeye, anayeweza kujua
tabia zijazo za mtoto wake.

Post a Comment