IGP SIRRO AWAITA NDUGU WA HAMZA KUUCHUKUA MWILI

 Hamza the gunman unmasked - The Citizen

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, (IGP) Simon Sirro amewataka ndugu wa Hamza Mohammed aliyeuawa na polisi kwenda kuuchukua mwili huo kwa kuwa wameshamaliza kuufanyia kazi.

Hamza aliuwawa Agosti 25, 2021 kwa kupigwa risasi na polisi dakika chache baada ya kuwaua askari polisi watatu na mlinzi wa kampuni binafsi karibu na ubalozi wa Ufaransa na daraja la Salenda jijini Dar es Salaam.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Agosti 28, 2021 wakati Jeshi la Polisi likiwaaga Makamishna wake, Balozi Valentino Mlowola na Robert Boaz amesema kuwa tayari wameshaufanyia kazi mwili huo hivyo ndugu zake wanaweza kwenda kuuchukua na wakishindwa mwili huo utazikwa na Halmashauri.

No comments