BIMA YA AFYA KWA WOTE YATENGEWA FEDHA
SERIKALI kupitia kwa msemaji wake
imeeleza kuanza kutekeleza Sheria ya Bima ya Afya kwa wote, ambapo imetenga
Fedha Shilingi Bilioni 149 kwa ajili ya mpango huo.
Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa ametoa kauli hiyo mjini
Dodoma katika mkutano wa Sita uliowakutanisha Wahariri wa vyombo vya habari na
mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Amesema mpango huo utatekelezwa baada ya muswada wake kufikishwa
bungeni mwezi Septemba mwaka huu ili kuwa Sheria rasmi na kuanza kutumika,
ambapo utaanza kwa kuwasaidia wananchi wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama za
matibabu.
Kwa Upande wake Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya Bernard Konga, amesema yapata miaka 20 tangu kuanzishwa kwa mfuko huo
ambao umewezesha kuboresha Sekta ya Afya kwenye Hospitali kubwa hapa nchini
pamoja na vituo mbalimbali vya Afya.

Post a Comment