DUCHU, AME WATOLEWA KWA MKOPO SIMBA


Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na maandishi yanayosema 'Protector Sabuni DUCHU 27 MO SIMBA FOUNDATION'

KLABU ya Simba imethibitisha kuwatoa kwa mkopo walinzi wake wawili vijana waliokosa nafasi katika kikosi cha kwanza.

Hao ni mlinzi wa kati Ibrahim Ame, aliyesajiliwa kutoka Coastal Union ya Tanga msimu uliopita ambaye amepelekewa Mtibwa Sugar na mlinzi wa pembeni kulia, David Kameta maarufu kama Duchu ambaye atakuwa na klabu ya Biashara United ya Mara ambayo pia itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho msimu huu.

 

No comments