BREAKING NEWS: Manchester United WATHIBITISHA KUREJEA KWA CRISTIANO RONALDO

KLABU ya Manchester United imethibitisha kumsaini tena nyota wake wa zamani Cristiano Ronaldo kutoka Juventus kwa dau la pauni milioni 19.4 saa chache baada ya kuonekana kama anajiandaa kutua kwa wapinzani wao, Man City baada ya simu kutoka kwa Sir Alex Ferguson na Rio Ferdinand.
Cristiano Ronaldo anarejea United kwa mkataba wa miaka
miwili na usajili huo umethibitishwa leo Ijumaa baada ya vipimo vya afya.
Kocha Ole Gunnar Solskjaer alisema Bruno Fernandes amekuwa
akizungumza na Ronaldo kuhusu mustakabali wake wa baadaye.
Unites iliwataarifu mashabiki wake kupitia mitandao
ya kijamii na ukurasa wao rasmi kuwa wamekubaliana na Ronaldo atarejea kuelekea
siku ya mwisho ya usajili.

Post a Comment