BINTI AVAA KAMA BARMAID NA KUMUIBUKIA MAMAKE GROCERY BAADA YA COVID KUWATENGANISHA KWA MIEZI 18

 Sophie Nugent surprised her mother, Emma, At a Leeds pub after not seeing each other for 18 months

BINTI mmoja nchini Uingereza amempa suprise mama yake baada ya kuvaa mavazi ya wahudumu wa baa na kumuibukia huku akiwa na kinywaji katika pub moja, miezi 18 baada ya kutoonana kutokana na vikwazo vya usafiri kutokana na janga la Covid 19.

Emma Nugent, wa Leeds, hakuwa amemuona bintiye Sophie, kwa miezi 18 kwani kwa kuishi kwake Qatar Sophie Nugent hakuwa na uwezo wa kumtembelea mama yake.

Mama alipatwa na mshtuko baada ya kumuona bintiye akiwa katika mavazi ya wahudumu akimletea kinywaji pale alipokuwa amekaa.

Mwalimu huyo Mhispaniola anayeishi Doha, Qatar, Sophie Nugent, na mumewe, hakuwa na uwezo wa kurejea England kutokana na vikwazo kwa zaidi ya mwaka kabla ya kuamua kurejea.

Alikata tiketi bila kuwataarifu ndugu zake na kumshangaza mama yake akiwa na baba yake wa kambo, Paul wakiwa wanapata kinywaji huko Rawdon, West Yorkshire. 

Dada yake, Sasha alipiga video tukio hilo wakati mdogo wake akiwa amevaa shati jeupe na suruali nyeusi pomoja na miwani kama walivyokuwa wamevaa wahudumu wengine na akawafuata akiwa amevaa kinyago usoni ili kuficha utambulisho wake.

Emma was visibly shocked when the waitress revealed herself to be Emma's daughter and gasped before getting up to give her a cuddle




No comments