WASANII WA WCB NA ALI KIBA JUKWAA MOJA?


I am the king,' Ali Kiba tells Diamond and Harmonize

YES. Ni katika Nandy Festival inayofanyika leo mjini Kigoma, katika eneo la Mwanga Centre ikiwa ni shoo ya kwanza ya tamasha hilo mwaka huu.

Na atakuwa ni msanii mwenyeji wa Kigoma, Baba Levo ndiye atapanda jukwaani akitokea WCB sambamba na mfalme wa Bongo Fleva, Alikiba, Whozu, Marioo, Linex na Nandy mwenyewe.

Kile kinachosemwa kuwa uhasama wa kimuziki baina ya wenyeji wawili wa Kigoma, Ali Kiba na Diamond Platnumz imefanya ionekane kama ni jambo gumu kwa wasanii wa pande hizo mbili kuweza kukutana katika jukwaa moja wakitoa burudani.

Akizungumzia uwepo wake katika shoo hiyo, Baba Levo ambaye pia ni mtangazaji wa Wasafi Fm, alisema amepata ruhusa kutoka kwa Big Boss Diamond ili afanye vitu vyake kwenye tamasha hilo.

"Uzuri nimepata go ahead kutoka kwa my Big Boss Diamond Platnumz nilikwenda kumuuliza kwamba nimepata show ya Nandy na Diamond akatoa baraka zote akasema nenda ka-perform 100%, hakikisha unafanya show nzuri kwa ajili ya kulinda brand, so nina uhakika 100% nitafanya show nzuri ya kulinda brand"

 

No comments