NDEGE YATUA BARABARANI KWA DHARURA

Picha siyo ya tukio la leo
SIJUI ingekuwaje kwa barabara zetu
kama ingetokea mitaa ya Mlandizi -Chalinze pale. Ndege ndogo aina ya Cessna 172
ikiwa na mwanafunzi wa urubani na mwalimu wake, imelazimika kutua barabarani
kwa dharura baada ya kugundulika kwa tatizo ikiwa angani.
Ujasiri, uzoefu na kutokuhaha ni
miongoni mwa vilivyosaidia kuishusha salama ndege hiyo ndogo na kutua nayo
kwenye barabara kuu baada ya kukosa nguvu ikiwa angani huko Agoura California
Marekani.
Wakiwa na dakika sita tu za kutafuta sehemu ya kutua Mwalimu
wa Urubani aliyekuwemo kwenye Ndege hiyo Captain Trevor Peterson ambae pia ni
Mwanajeshi wa Marekani ilibidi amuweke pembeni Mwanafunzi na kuishusha Ndege
salama.

Post a Comment