MANJI AACHIWA KWA DHAMANA TOKA TAKUKURU


Dailynews

 MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yussuf Mehboob Manji, ambaye aliwasili nchini siku chache akitokea Ughaibuni alikoenda tangu mwaka 2018, ameachiwa kwa dhamana kutoka mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU.

Bosi wa Taasisi hiyo, Kamanda Hamduni amethibitisha jambo hilo, hata hivyo akisema pamoja na kuwa nje kwa dhamana, bado wanaendelea kuchunguza tuhuma dhidi yake.

Pamoja na mambo mengine, Manji anadaiwa kukwepa kodi kupitia kampuni zake kadhaa zilizopo nchini.

No comments