UCHAGUZI MKUU TFF AGOSTI 7 MWAKA HUU


Wallace Karia rais mpya TFF | Goal.com

SHIRIKISHO la soka Tanzania, TFF limetangaza kwamba Uchaguzi Mkuu utafanyika Agosti 7 mwaka huu, jijini Tanga.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, imesema katika uchaguzi huo, nafasi zitakazogombewa ni moja ya Urais na sita za wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Kwa nafasi ya Urais, taarifa imesema mgombea anapaswa kuchukua fomu kwa ada ya shilingi laki tano, wakati wale wa ujumbe, watalazimika kulipia laki mbili kila mmoja.

Rais wa sasa wa TFF, Wallace Karia amesema atatetea tena nafasi yake na hadi sasa hakuna fununu ya mwingine anayetaka nafasi hiyo. Mgombea wa nafasi hiyo msimu uliopita, Ally Mayai amesema hatagombea safasi hii.

No comments