UBAGUZI WAONDOA UHAI WA KINDA WA SOKA ITALIA


Debate on racism after the suicide of Seid Visin

UBAGUZI wa rangi..Tabia ya wazungu kuwabagua waafrika umeendelea na safari hii umeshindwa kuhimili uvumilivu kwa kijana Seid Visin kuamua kujiua baada ya kudhalilishwa kila kona akiwa nchini Italia.

Seid Vision amewahi kuichezea timu ya vijana ya AC Milan.

Kabla ya kuamua kujitoa roho, mwanasoka huyo aliyekufa akiwa na umri wa miaka 20 tu aliandika;

"Sikuja nchini Italia kwa kupenda bali nilichukuliwa kutoka nyumbani Ethiopia na wazazi wawili wa Kiitaliano (Adoption) wakanileta huku kama mtoto wao.

"Mwanzoni maisha nchini Italia yalikuwa mazuri na kila mtu alinipenda ila mambo yalianza kubadilika punde baada ya kupata ajira ya kufanya kazi hotelini.

"Wateja walisusia huduma yangu, wengi niliowahudumia walinifukuza kama Mbwa, huko viwanjani pia kila siku ilikuwa ni ubaguzi dhidi ya rangi yangu na Uafrika wangu.

"Nilitengwa kila sehemu, haswa watoto wa Kiitaliano ambao hawana kazi ila mimi sikuwahi kuchagua kazi, hivyo nimeamua kukatisha maisha yangu kwa kuwa sina wa kumlilia wala wa kunisaidia."


No comments