T.B JOSHUA AFARIKI DUNIA

TANZIA! Mchungaji na muombezi maarufu barani Afrika, Temitope Balogun Joshua, anayefahamika zaidi kama TB Joshua, amefariki dunia.
Mchungaji huyo muasisi wa kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) anadaiwa kufariki Jumamosi jioni, muda mchache tu baada ya kumaliza kutoa huduma kwa waumini wa kanisa lake.
Chanzo cha kifo cha mchungaji huyo aliyezaliwa Juni 12 mwaka 1963 hakijatajwa.
TB Joshua alijijengea
umaarufu mkubwa duniani, hasa kusanyiko lake la kila mwaka ambalo hufanyika
huko Nigeria, kwa wafuasi kutoka kote duniani kwenda kusali pamoja naye.

Post a Comment